MAMBO 9 YA KUZINGATIA UNAPOKWENDA KUONANA NA MPENZI WAKO KWA MARA YA KWANZA
Unapokwenda kuonana na
mpenzi wako kwa mara ya kwanza, namna utakavyokuwa ukionekana, inamaana
kubwa sana. Ukweli ni kuwa muonekanao wako, namna ulivyovaa unaweza
kuamu kama utapewa nafasi ya ‘second date’, hivyo vaa vizuri na pendeza.
Kama unakwenda kwenye
‘date’ alafu uko rafu rafu tu, hii inatoa ujumbe kwa mwenza wako kuwa
humjali na kuwa vyovyote utakavyovaa kwako wewe ni sawa.
Basi, ni namna gani ya mwanaume unaweza na ukapendeza unapokwenda kuonana na mpenzi wako mara ya kwanza?
1. Usivae nguo za kukubana sana
Ukivaa suruali
inayokubana itakunyima kukaa kwa uhuru, mara uipandishe, huwezi kupiga
hatua vizuri, mwisho wa siku unaweza kujikuta umeharibu usiku wako na
mpenzi wako kwa sababu ya nguo inayokufanya usiwe huru
2. Kuwa mtanashati
Hakikisha kama umevaa
shati umelipasi limenyooka vizuri, nywele umechana sawia, kucha umekata
vizuri, hili litamfanya mpenzi wako akuona namna ulivyo ‘smart’ na
muajibikaji.
3. Usithubutu kuvaa mtindo ambao hujawahi kuuva kabla
Unapotaka kutoka, usivae
mtindo mpya wa nguo, kuwa halisi, kuwa wewe, vaa kama unavyovaa mara
zote. Kumbuka kuwa jinsi unavyovaa huelezea wewe ni mtu wa aina gani, na
kama sio kawaida yako kuvaa mtindo huo uliouchagua atagundua tu.
4. Usiweke vikorombwezo vikazidi
Watoto wa mjini wanasema
‘keep it simple’, huna haja ya kuvaa michezi, mipete, misaa kibao uanze
kuwa kama mwanamuziki wa Marekani. Ukivaa saa moja tu mkononi inatosha.
5. Usivae nguo zenye maandishi
Kuvaa nguo zenye
maandishi kwenye ‘date’ kwa mara ya kwanza kuna hatari mbili, moja
utaonekana kuwa haupo ‘serious’ kutokana na ujumbe uliopo kwenye nguo
yako lakini pili, ujumbe unaweza kumkera mwenzako.
6. Marashi
Kujiweka smart unahitaji
na marashi ili unukie mwanana, lakini sasa yasizidi kiasi kwamba
ukifika mahali kila mtu anafunika pua sababu unawasababishia mafua. Hii
itafanya usiku wako kuwa mbaya, jipulizie marashi ila kwa kiasi.
8. Rangi ya nguo
Chagua rangi ya nguo ambayo itavutia na pia itakayoendana na mazingira, sio unavaa nguo inang’aa kama ‘reflector’ ya gari.
9. Usivae miwani au kofia ambazo zitakufunika uso kiasi kwamba mtu akitaka kukuona usoni hadi ainame chini.

No comments: