MAKALA: SABABU YA WANAWAKE KUPENDA KUFANYA MAPENZI GIZANI
Inaeleweka kuwa wapendanao iwe wanandoa au wapenzi hupenda kufanya mapenzi sehemu yenye mwanga hafifu au gizani.
Tofauti na watu na mataifa mengine, kwa Waafrika suala hilo ni siri na linahitaji faragha kukamilika.
Lakini kwa baadhi ya
watu imekuwa kero kutokana na kutamani kufanya tendo hilo gizani, huku
wanawake wakitajwa kuwa vinara wa kuzima taa.
Utafiti mpya umebaini
kuwa katika kila wanawake wanne, mmoja anapenda na anakuwa huru kufanya
mapenzi gizani kwa sababu mbalimbali ikiwamo kutojiamini. Carl Loudgers
aliyeshiriki kwenye utafiti huo na kuwauliza wanawake zaidi ya 2,000 kwa
kukusanya majibu kwa njia ya mtandao anasema walibaini asilimia 60 ya
wanawake hao wanatamani kuwa na ujasiri wa kukutana kwenye mwanga lakini
wanashindwa.
Anasema zaidi ya asilimia 75 walisema hawapendi miili yao, huku asilimia 66 wakisema wanaona aibu kutokana na mwonekano wao.
Utafiti huo uliofanywa
na mtandao wa Weight Watchers, ulibaini asilimia 27 wanafanya mapenzi
gizani kwa sababu hawaamini miili yao kama inavutia kwenye mapenzi.
Ulionyesha pia asilimia
38 ya wanawake na wanaume waliohojiwa walisema kuwa wanaamini wapenzi
wao hawatawaona wanavutia wakiwa watupu.
Sheiilar Gregam miongoni
mwa wanandoa waliohojiwa kwenye utafiti huo alisema jambo linalochangia
hali hiyo ni mitandao. Alisema wanawake wanaoonekana wakiwa watupu
kwenye mitandao ni wale wanaovutia kiasi ukijilinganisha nao inakuwa
ngumu kukubali kukaa bila mavazi, huku wapo ambao wanavutia.
“Nikiangalia mastaa
walivyo na maumbile ya kuvutia, baadhi yao wamezaa, natambua kuwa wapo
wanaojirudishia wakiharibika kama mimi baada ya kuzaa, lakini nakosa
kujiamini kabisa na ninaamini hao wanapendeza zaidi yangu,” alisema
Sheiilar katika mahojiano ya utafiti huo.
Baadhi yao wamekuwa wakiona aibu ya vitu vilivyomo mwilini mwao kama matiti, alama za mwilini na makovu ya upasuaji.
Maziwa kuanguka baada ya kunyonyesha mara tatu.
Kuning’inia nyama za
tumbo na kuongezeka uzito ni moja ya sababu za kuzima taa. Matokeo ya
utafiti huo pia umebaini wanawake wawili katika kila wanawake watatu
huchukia kuangalia wanawake wenzao wakiwa hawajavaa nguo.
Ulibaini kuwa asilimia 60 ya wanawake hawapendi kabisa kujitizama wao wenyewe kwenye kioo wakati wa kuvua nguo.
Loveness Ayoub mkazi wa
Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam anasema hupata wakati mgumu
anapokutana na mwanaume mzuri kwa sababu hukosa kujiamini na hivyo
hufurahia zaidi wakijamiiana gizani.
Anasema akijitizama na
rafiki zake humwambia amenenepa, hivyo akiwa na mwanaume anayevutia
huamini atamuacha kutokana na umbo lake lilivyo.
“Tangu nipo chuo rafiki
zangu walikuwa wananishangaa nikivua nguo, kiasi kwamba sikuwa nafanya
hivyo wakiwepo, hali hiyo imenijengea uwoga na kunipotezea kujiamini.
“Nikiwa na mwanaume mtu
mzima huwa sijali kwa sababu naamini ameona wanawake wengi amekuja
kwangu kwa ajili ya kupumzika na sihitaji kuwa naye maishani
ukilinganisha na wanaovutia ambao natamani hata wanioe,” anasema Ayoub.
“Nimeoa nina watoto
wawili na huyo mke wangu, lakini nikitaka kumuona vizuri umbo lake akiwa
mtupu nimvizie anaumwa au kalala, tofauti na hapo hajawahi kuvua nguo
akakaa mbele yangu,” anasema Omari Kiyungi. Kiyungi anasema licha ya
kuishi pamoja kwa zaidi ya miaka tisa mkewe hataki kabisa kukaa mtupu
mbele yake kwa madai ya kuona aibu.
“Sipendi, natamani
nimuone akiwa hajajiziba na ‘manguo’, lakini juhudi zangu zimegonga
mwamba, hana dalili hiyo na hataki kabisa,” anasema.
Anasema alikuwa
anachukia hadi sasa amezoea na akimuona mwanamke amevaa kihasara hasara
anamdharau na kumuona hajiheshimu kwa sababu amezoea kufichiwa maungo.
Alisema akitizama mwili wake kwenye kioo hasa baada ya kuzaa mara mbili
na kunenepa huogopa na kuhisi anamuangusha mumewe kwa umbile lake.
Msimamizi mkuu wa
utafiti huo na mshauri wa masuala ya saikolojia Keren Smedley alisema
wengi wa waliobainika kuona aibu kuvua nguo mbele ya wapenzi wao
hawakuwa na tatizo na walikuwa na kila sifa ya kumshawishi mtu
kuwatizama.
Akizungumzia hali hiyo
mfundaji kutoka Mbagala Charambe, Zakia Kilimi maarufu Mchambaji,
anasema wanawake wamekuwa na hali hiyo kutokana na tamaduni za siku za
nyuma kuwa mapenzi hufanywa kwa siri.
Anasema wakati huo hasa
kwa familia za kawaida walikuwa wanaishi katika chumba kimoja, hivyo
upende usipende utazungumza na mwenzi wako gizani.
“Hii hali imesababisha
hata wanawake wengi kushindwai kuachia hisia zao kwa wapenzi wao
wakiamini wataonekana malaya na wasio na maadili kwa sababu imezoeleka
mambo hayo ni ya kunyata nyata,” anafafanua.
Anaongeza kuwa siku hizi
hayo mambo ndiyo yanakwisha na wanawake bila kujali wana umbo zuri,
baya, makovu wanajiachia na kutambua umuhimu wa faragha ni kuonana hivyo
wazazi wasiwatishe watoto wa kike kuwa kujiachia ni uhuni.
Zainabu Jumanne (siyo
jina lake halisi) anasema kuwa mpenzi wake anajivunia kuwa naye lakini
wakiwa faragha anashindwa kukaa mtupu. Anasema vivyo hivyo hata
wanapojamiiana kukiwa giza hufanya kila aina ya mbwembwe tofauti taa
ikiwa inawaka.
Anafafanua kwa sababu hiyo mumewe akitaka kuburudika na kukata kiu ya kuzungumza naye faragha huzima taa kabla hajaambiwa.
“Sijiamini kabisa kukiwa na taa, nahisi kama ananichora ninavyoweweseka, lakini kukiwa giza ashindwe yeye tu,” anasema.
Anaitaja sababu nyingine
ya kupenda kujamiiana gizani ni matiti yake yamelala halafu hayana
nyama. Anasema anatumia ufundi wa faragha kuziba yote hayo kwa
kumuonyesha mitindo mipya, lakini ili ayapate hayo sharti iwe gizani.
“Kukiwa giza akakubali
kukutana nami, akiniacha nitatambika sina historia ya kuachwa tangu
nikiwa msichana hadi nimeolewa, ingekuwa najiamini na kujamiiana kwenye
mwanga na mautundu niliyonayo, naamini ningekuwa mkali zaidi, nimejaribu
nimeshindwa na kwa hapa nilipofika haiwezekani tena,” anasema.
Mkazi wa Tandika jijini
Dar es Salaam, Yusufali Yusuph anasema hataki hata kumsogelea mwanamke
anayependa kujamiiana gizani kwa sababu huamini kuna kitu anaficha.
Anasema siku hizi maradhi mengi, anaweza kudhani anaona aibu au hajazoea kumbe kuna jambo anaficha.
“Haa raha ya mapenzi muonane jamani gizani tena! Siwezi na simtaki mwanamke wa aina hiyo,” anasema Yusuph.
Mtaalamu wa masuala ya
saikolojia Modester Kamongi anasema yapo mambo mengi yanayochangia
mwanamke kuogopa ikiwamo kutokujiamini.
Anasema mila, desturi na
tamaduni ni miongoni mwa mambo yanayochochea hilo kwa sababu wanawake
wengi huamini stara ndiyo sifa ya kuwa mke bora na kushindwa
kutofautisha mahali pa kujistiri pa kujiachia.
Kamongi anasema
linapokuja suala la aibu siyo kwa wanawake pekee wapo wanaume wenye aibu
na wameumbwa hivyo, ikitokea kukutana na mmoja wa watu hao cha kufanya
ni kuwazowesha taratibu hatimaye kama binadamu watakubaliana na hali
halisi japo kwa shida.
“Huwachukua muda kuzoea,
lakini uwezekanao upo na wakasahau kabisa kama walikuwa hawawezi,
lakini inahitaji utayari wa kuwazowesha badala ya kuwalazimisha,
”alisema Kamongi.
Anaitaja sababu nyingine inayochangia wanawake kukataa kukaa utupu kuwa ni kutojiamini.
Anasema hali hii hutokana na maneno anayosikia au aliyosoma kuhusu umbo lake.
Anafafanua kuwa kuna
baadhi ya familia mtoto akiwa mnene au mwembamba au ana umbo fulani
uhusisha umbo hilo na neno ukiolewa sijui itakuwaje.
“Mtoto hukuwa na neno au
misemo ya aina hiyo hivyo anapoolewa au kuwa na mpenzi hukumbuka na
kutamani asimuone kwa sababu hajui itakuwaje kama alivyokuwa anaambiwa.
“Wengine hudhani
mwanaume akiona umbile lake ambalo lilikuwa linawaisha ndugu, rafiki
zake litamtisha pia na kuamua kumuacha, hivyo huona afadhali nusu shari
kuliko shari kamili ya kuachwa,” anasema Kamongi.
Anaeleza wote hao
wanaweza kubadilika iwapo wataeleweshwa na kujengewa kujiamini ikiwamo
kwa kusifiwa kila wanapokaa bila nguo hata kwa bahati mbaya.
“Wengi wao hawajiamini,
wakisifiwa na muhusika kuonyesha kutamani kuona maumbile yao mazuri
yakiwa wazi taratibu watabadilika,” anasema.
Ushauri wazazi wawajenge
watoto wa kike kuthamini vile alivyo navyo hususan kuukubali mwili wake
badala ya kuwasema kwa ubaya kwa eneo lolote la mwili lililozidi au
kupungua.

No comments: